Mourinho alifanya mabadiliko ya wachezaji nane kwenye kikosi kilichocheza mechi ya Alhamisi ambapo walicheza vibaya na kufungwa 1-0. Bao lilifungwa na Tonny Vilhena dakika ya 79.
Nahodha Wayne Rooney na wachezaji wengeine Antonio Valencia na Luke Shaw walipumzishwa kwa ajili ya mechi hiyo ya Ligi ya Premia itakayochezwa Jumapili.
Mourinho amesema: “Tunarejelea kikosi cha kawaida bila mabadiliko makubwa.”
Paul Pogba alikuwepo safu ya kati lakini hakuweza kutamba.
“Huwa sitaki kuangalia wachezaji binafsi sana,” amesema Mourinho . “Ni jambo nisilopenda.”
“Nafikiri ni kama alicheza kama timu yote. Kipindi cha kwanza walidhiti mechi lakini kasi yao ilikuwa nusu. Kipindi cha pili waliongeza kasi na hapo ndipo tulifungwa.”
Note: Only a member of this blog may post a comment.