Tuesday, March 8, 2016

Anonymous

VIGOGO Ligi Kuu Uingereza Waangukia Pua Kwa VARDY!

Timu inayoshika usukani wa kuongoza ligi kuu ya Uingereza, Leicester City imetangaza kuwa thamani ya Vardy ni paundi milioni 30 kwa timu ambazo zinazomtaka kumsajili mchezaji huyo.

Leicester City ambayo inaongoza ligi kuu ya Uingereza ikiwa na pointi 60, huku wakipewa nafasi kubwa ya kuchukuwa kombe hilo la ligi kuu nchini humo. Vigogo wa ligi hiyo tayari wameshakata tamaa ya kuwania kombe hilo.

Mpaka sasa Vardy, 29 ameshaifungia timu yake ya Leicester magoli 19 kwenye mashindano yote ambayo timu hiyo imeshiriki msimu huu. Mkataba wa Vardy unaisha 2019 baada ya hivi karibuni kusaini mkataba wa miaka mitatu ambao unamfanya alipwe paundi 80,000 kwa wiki.

Timu za Chealsea, Manchester United na wengine wanaonekana kumnyatia mchezaji huyo kutokana na kuvutiwa na ufungaji wake bora wa magoli na uchezaji wake mzuri wa kujiamini akiwa uwanjani.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.