Tuesday, July 5, 2016

Unknown

Ufafanuzi Kuhusu Picha Iliyosambaa ya Kumdhalilisha RC Paul MAKONDA

Paul Makonda.
Pio Pius
MH MAKONDA vs MASHOGA ( Ufafanuzi wa Picha iliyosambaa).
Baada ya kuona ile picha ikimuonyesha Mkuu wa Mkoa Mh Paul Makonda akiwa kwenye Sanamu lililo uchi(Naked Statue), nimefanya uchunguzi wangu personally na nimegundua Mambo yafuatayo.

1. Picha ile inayomuonyesha Mh Makonda yuko pembeni ya hilo sanamu la Uchi nimeifatilia kwa makini na uchunguzi wa hali ya juu ili kujiridhisha kama kuna ukweli wowote,....but finally nimegundua kwamba picha hiyo ni ya Ku-edit, yaani wamechukua picha moja ya Mkuu wa Mkoa akiwa kwenye Hafla ya Kitaifa....kisha Wakaenda kumbandika pembeni ya picha ya sanamu naked man Mongolian Statue.

2. Hapo pichani ni ushahidi tu wa nilichoelezea hapo juu...hapo ni katika bustani ya Chuo Kikuu cha Peking nchini China(Peking Universty),...bustani hiyo ipo mbele ya Guanghua School of Management kuna sanamu la Mongolian Statue, na pia Ukienda Paris napo lipo sanamu kama hilo, sasa kwa kuwa lile sanamu la Paris ndilo ambalo wafanya editing wamelitumia katika picha hebu tuone vipimo: Mongolian Statue Paris (Sanamu) lina urefu wa karibu futi 13.8 lenyewe bila msingi,..na msingi wake una urefu wa takribani futi 2.5 na kwa jumla ni zaidi ya futi 16.3 kutoka chini kwenye Msingi hadi juu, sasa kwenye Picha inaonekana Mh Makonda amelifikia kiunoni, je ina maana Mkuu wa Mkoa ana Urefu wa Futi 8? yaani zaidi ya Hasheem Thabeet wa NBA mwenye 7.3ft? ... Zaidi ya Mchina Yao Ming mwenye 7.6ft?...Mama wee! Amekuwa Ngongoti? Au alisimama juu ya Stuli ndefu ya kukatia michongoma?

3. Mfanya Editing amejitahidi kudanganya lakini kachemsha kuanzia kwenye Allocation, Contrast, n.k na ndio maana kashindwa kuweka full picture tuone mpaka miguuni,..maana sio kawaida Mtalii apige selfie au half picture na sanamu...hakika huyu Editor wa picha Jela inamuita, ajiandae!
Naamini Vyombo vya Usalama vitafanyia kazi swala hili, sasa Manabii wa Matusi na edit za kipuuzi wataanza kupaa mdogo mdogo kuelekea Segerea,

Kifupi sijaposti ile picha ya editing ya Mheshimiwa kama reference kwa Sababu natambua ku-share au ku-posti picha hiyo ya uongo na inayomdhalilisha Mkuu wa Mkoa ni Criminal offense, hii kesi haina tofauti na kukutwa na Cocaine gunia 2. Mwisho niseme Wazi Juhudi za Aidha Mashoga katika kudai haki za Ushoga ndani ya nchi isiyo Signatory katika Ushoga hazikubaliki, pia juhudi za Siasa chafu naona zinaendelea kugonga mwamba... Narejea kusema hizi ni Siasa za Kipuuzi.

Tafadhali nawaasa ndugu, jamaa na Marafiki msiendelee kushea au kuposti picha iliyofanyiwa editing na mtu ambaye muda si mrefu atatiwa katika Mikono salama... Mikono ya kupata Ugali bure na Maharage bure pale Segerea, its a Criminal Offense.
Pio Pius@2016

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.