Saturday, May 14, 2016

Anonymous

PICHAZ 17: Tazama YANGA SC Walivyopokea Kombe Lao la Ligi Kuu Msimu wa 2015/2016 Leo May 14 2016


Ligi Kuu soka Tanzania bara imeendelea kwa Bingwa wa Ligi Kuu klabu ya Dar es Salaam Young Africans kucheza mchezo wake wa 29 dhidi ya Ndanda FC uwanja wa Taifa Dar es Salaam, licha ya kuwa Yanga tumezoea kumuona Taifa kama mwenyeji ila leo yeye ndio alikuwa mgeni wa Ndanda FC ambao walikubali kuchezea Taifa kama uwanja wa nyumbani.

Katika mchezo huo wa kukamilisha ratiba ya Ligi Kuu klabu ya Dar es Salaam Young Africans ambao ndio Mabingwa wa Ligi Kuu kwa kutetea taji hilo mara mbili mfululizo, wamelazimishes sare ya goli 2-2, Ndanda FC ndio walianza kufunga goli kwa mkwaju wa penati dakika ya 28 kupitia kwa Omary Mponda.

Yanga walifanikiwa kusawazisha goli dakika ya 36 kupitia kwa Simon Msuva, lakini dakika ya 40 Donald Ngoma akapachika goli la pili kwa Yanga na kuwafanya Yanga kuwa mbele kwa goli 2-1, Yanga waliendelea kuutawala mchezo katika uwanja ambao umejaa mashabiki wake ambao wanasubiria kuona Kombe lilikabidhiwa, kujisahau kwa Yanga kuliwafanya Ndanda FC kuchomoa goli dakika ya 80 kupitia kwa Atupele Green.













USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.