Rappa Dogo Janja amewataka vijana kujituma katika nafasi zao za kazi ili kukuza vipato vyao huku akidai maisha ni akili vingine ni mbwembwe.
“Maisha yamebadilika sana, ubunifu, ujanja ujanja, watu wajue maisha ni akili vingine mbwembwe,” alisema Dogo Janja.
“Kikubwa ni kujituma sana, vijana wafanye kazi kwa bidii ndiyo maana nikasema maisha ni akili vingine mbwembwe, kwa sababu ukijiongeza tu, kila kitu kinawezekana,” aliongeza Dogo Janja.
Rapa huyo ambaye anafanya vizuri na video yake ya wimbo ‘My Life’, amewataka mashabiki wa muziki wake kubiria kazi mpya hivi karibuni.
-Bongo5
Note: Only a member of this blog may post a comment.