Mkuu wa jeshi la polisi Nigeria ametibitisha taarifa hizo japo hakutoa maelezo mengine ya ziada. Taarifa zimeripotiwa siku mbili baada ya kupatikana kwa msichana mwingine wa kundi hilo la Chibok girls Amina Ali.
Amina Ali ambaye alipatikana May 18 2016 alialikwa na Rais wa Nigeria nyumbani kwake akiwa pamoja na mama na mtoto wake aliyejifungua wakati akiwa mateka wa kundi la kigaidi la Boko Haram, anasema kati ya wanafunzi wenzake, sita walipoteza maisha walipokua mateka.

Note: Only a member of this blog may post a comment.