Kwa namna ambavyo hali ya kisiasa ya vyama vya upinzani inavyozidi kupoteza mvuto mbele ya jamii kipindi hiki cha utawala wa awamu ya tano,huenda unabii wa Profesa Kitila ukatimia.
Muda mfupi mara tu baada ya utendaji uliotukuka wa serikali ya CCM chini ya Dr Magufuli,Prof Kitila mkumbo aliandika kupitia account yake ya twitter na hapa namnukuu;
"Tunahitaji upinzani utakaojikita katika sera mbadala.Upinzani unaotegemea makosa ya serikali ya CCM pekee unaweza kupwaya sana kipindi hiki",mwisho wakumnukuu.
Nafikiri kwa hali ilivyo sasa juu ya taswira ya siasa za vyama vya upinzani nchini ilivyo ni dhahiri utabiri huu unajidhihirisha kwani ni kweli wapinzani hasa CDM walizoea sana siasa za matukio ili kuimarisha chama.
Lakini prof Kitila Mkumbo hakuishia hapo kutoa tahadhari kwa vyama vya upinzani,siku nyingine kupitia account yake ya twitter aliandika tena na hapa namnukuu,
"Upinzani uchwara hushamiri sana wakati wa serikali dhaifu.Upinzani makini huibuka wakati wa serikali makini na yenye chembe ya udikteta",mwisho wa kumnukuu.
Nafikiri kama wapinzani hawataacha siasa za kuishi kwa matukio kama walivyozoea CHADEMA,Kipindi hiki cha utawa wa CCM chini ya Magufuli huenda tukashuhudia anguko kubwa la vyama vya upinzani nchini.
Imeandikwa na Gimmy's

Note: Only a member of this blog may post a comment.