AUNT EZEKIEL.
Na Gladness Mallya
Kuna watu wamekuwa wakisema kuwa, duniani hakuna mtu aliyeumbwa mwembamba! Kwamba unayemuona leo akiwa mwembamba usije ukashangaa kesho ukakutana naye akiwa bonge kiasi cha kuchukiza.
Hilo limekuwa likitokea sana kwa wanaume na wanawake. Mifano ya watu hao ipo na tunapoiangalia fani ya uigizaji Bongo, wapo mastaa wa kike ambao huko nyuma walikuwa potabo, lakini leo hii wamekuwa mabonge kiasi cha baadhi yao kujichukia.
Wanajichukia kwa sababu wanajua kwa ubonge wao umepunguza na urembo wao pia. Wamejiachia kwa kula mapochopocho, kunywa pombe sana huku wakitumia muda mwingi kulala na kusahau mazoezi.
Mazingira yamewafanya wakose madili ya kuigiza kwenye filamu ambazo zinawahitaji wasichana warembo. Yaani kuna ‘scene’ ambazo zamani walikuwa wakizicheza vizuri lakini leo hii hawawezi kupewa shavu kwa sababu ya unene unaowakosesha mvuto na hivyo kuingia grupu la wamama.

BLANDINA CHAGULA ‘JOHARI’.
Wanakosa sifa ya ku-maintain muonekano wao kutokana na kushindwa
kufuata ratiba ya vyakula kwa mujibu wa fani yao. Katika makala haya,
mwandishi wetu anakuletea baadhi ya mastaa ambao maumbo yao kwa sasa
yapo tofauti na zamani.
AUNT EZEKIEL
Amejaliwa kuwa na mtoto mmoja wa kike aitwaye Cookie. Kwa sasa amekuwa
bonge kupita kiasi kwani muonekano wake wa zamani, ule wa Ki- Miss,
uliowahi kumfanya wakati f’lani kuwa mshindi wa shindano la urembo
mkoani Mwanza, limepotea kabisa. Amepoteza sifa zake za urembo.
WEMA SEPETU
Mwanadada huyu ambaye ni Miss Tanzania mwaka 2006 na mcheza filamu za
Kibongo, amebadilisha kabisa muonekano wa mwili wake, kwani hivi sasa
amenenepa tofauti na enzi zake.
BLANDINA CHAGULA ‘JOHARI’
Staa huyu mkongwe kwenye gemu la filamu wakati anaigiza filamu ya kwanza
kabisa ya Johari, alikuwa na umbo f’lani ‘amaizing’ lakini kwa sasa
amefutuka na kuwa mnene.
JACK PENTZEL ‘JACK CHUZ’
Msanii huyu ambaye ni mama wa mtoto mmoja, zamani alikuwa mwembamba
kiasi lakini kwa sasa amekuwa mama, kwani amejiachia na kunenepa sana
hali iliyopoteza kabisa ule muonekano wake wa zamani.
LULU SEMAGONGO ‘AUNTY LULU’.
LULU SEMAGONGO ‘AUNTY LULU’
Dada huyu asiyeishiwa matukio, aliyepata umaarufu tangu akiwa mtoto, pale alipokuwa mtangazaji wa Kipindi cha Watoto Show cha Radio One, muonekano wa mwili wake umebadilika kwa kiwango kikubwa sana.
Licha ya kuwa ni mtangazaji, pia ni muigizaji wa filamu za Kibongo, zamani alikuwa mwembamba sana lakini kwa sasa amekuwa bonge na kila anakopita wanaume wakware lazima wakate shingo zao kumtazama.
TIKO HASSAN
Ni mama wa mtoto mmoja, kwa sasa amejazia tofauti na zamani kwani alikuwa mwembamba jambo ambalo linawafanya watu wamshangae kutokana na ubonge wake uliokuja ghafla.

Note: Only a member of this blog may post a comment.