Friday, April 1, 2016

Anonymous

MAGUFULI Amponza 'Mlevi', Apandishwa Kizimbani Kwa Tuhuma za Kumtishia Kifo Rais MAGUFULI

HAMIMU Seif, mkazi wa Mwananyamala Ujiji, Dar es Salaam, amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Kisutu akituhumiwa kumtishia kifo Rais John Magufuli, anaandika Faki Sosi.

Mbele ya Hakimu Mkazi Helleni Liwa, Keneth Sekwao, Wakili wa Serikali, aliiambia mahakama kuwa kijana huyo alitishia kumuua rais Machi 10 mwaka huu, alipokuwa katika baa ya Soweto maeneo ya Makumbusho, Jijini Dar es Salaam.

Sekwao ameeleza mahakama kuwa kijana huyo alitamka kuwa amechoshwa na mambo anayofanya rais, na kwamba yupo tayari kujitoa mhanga kwa kujilipua na bomu.

Mshitakiwa amekana mashitaka, na mahakama imeweka wazi dhamana yake.
Kesi hiyo itatajwa tena mahakamani hapo tarehe 14 Aprili mwaka huu.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.