Kajala Masanja
Na Imelda Mtema
Siku chache baada ya gazeti dada na hili, Risasi Jumamosi kuandika juu ya aliyekuwa kigogo wa msanii Wema Sepetu, Clement Kiondo ‘CK’ kunaswa akiuza mishikaki, tukio hilo limemliza shosti wa Wema, Kajala Masanja.

Kumwaga chozi kwa Kajala kumetokana na maelezo yake kwamba, baada ya
kuiona habari hiyo hakuweza kuamini kama kweli ni CK yule aliyewahi
kumtolea shilingi milioni 13 kama faini ili asiende jela kutokana msala
aliokuwa nao.
Akizunbumza na Ijumaa kwa majonzi, Kajala alisema: “Kiukweli nililia
sana, nilishindwa kuamini kama kweli CK amefikia hali hiyo,” alisema
Kajala ambaye pia aliwahi kudaiwa kutoka kimapenzi na jamaa huyo.
Akasema stori hiyo isingekuwa imeambatana na picha asingeamini lakini
alipoona zile picha zinazomuonesha CK akiwa jikoni akimhudumia mtu,
alishindwa kujizuia na kujikuta akibubujikwa na machozi.
Tukio
la kunaswa kwa CK akiuza mishikaki lilinaswa na mapaparazi wetu
juzikati kwenye baa moja iliyopo maeneo ya Leaders Club, Kinondoni
jijini Dar, jambo lililozua maswali mengi kutokana na jeuri ya fedha
aliyokuwa nayo kigogo huyo.
Note: Only a member of this blog may post a comment.