Eluedi Misheto akiwa hospitali baada ya kujeruhiwa na mwalimu huyo.
Stori: Issa Mnally na Makongoro Oging’, UWAZI
PWANI: Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Baobab, Wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani nusura waibue timbwili kutokana na mwenzao kuadhibiwa na kujeruhiwa vibaya kwa madai ya kukutwa na laini ya simu.
PWANI: Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Baobab, Wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani nusura waibue timbwili kutokana na mwenzao kuadhibiwa na kujeruhiwa vibaya kwa madai ya kukutwa na laini ya simu.
Kwa mujibu wa baadhi ya wanafunzi, mwalimu mmoja ambaye jina
linahifadhiwa kwa sasa, alitoa adhabu hiyo kwa denti Eluedi Misheto wa
kidato cha sita hivi karibuni hali iliyomsababishia majeraha kadhaa
mwilini.
Ilidaiwa kuwa, denti huyo aliadhibiwa baada ya kukutwa na laini hiyo ya simu jambo ambalo inasemekana ni kinyume na sheria za shule hiyo.
Ilidaiwa kuwa, denti huyo aliadhibiwa baada ya kukutwa na laini hiyo ya simu jambo ambalo inasemekana ni kinyume na sheria za shule hiyo.
….Jeraha la begani.
“Baada ya kubainika ana laini ya simu, alipigwa kwa fimbo nene, damu
zilimtoka hali iliyoamsha hasira kwa wanafunzi wenzake na kutaka
kuanzisha vurugu, ikabidi uongozi wa shule ukimbilie Kituo cha Polisi
Mpinga wilayani Bagamoyo kuripoti.
Hata hivyo, inadaiwa kuwa amani shuleni hapo haijasimama sawasawa
kutokana na tukio hilo huku wanafunzi wakiutaka uongozi wa shule kutoa
tamko.
“Kinachotuuma ni kitendo cha kujeruhiwa mwenzetu na wala hakupelekwa
hospitali bali walimrudisha kwao akajiuguze. Hatuna amani hapa.”
Baba mzazi wa mwanafunzi huyo, John Misheto kwa upande wake alisema ameshangazwa na kitendo hicho cha kuadhibiwa mwanaye kiasi hicho na kisha kutelekezwa bila kupatiwa matibabu.
Baba mzazi wa mwanafunzi huyo, John Misheto kwa upande wake alisema ameshangazwa na kitendo hicho cha kuadhibiwa mwanaye kiasi hicho na kisha kutelekezwa bila kupatiwa matibabu.
Mmiliki wa shule hiyo ambaye pia ni mkurugenzi, Halfani Swai
alipohojiwa na Uwazi wiki iliyopita kwenye ofisi yake iliyopo eneo la
shule, alisema kuwa kuna tukio la wanafunzi kutaka kuleta vurugu na
walitoa taarifa polisi lakini hakufafanua ni hatua gani iliyochukuliwa
dhidi ya mwalimu aliyekiuka sheria na kumjeruhi mwanafunzi huyo.
“Baadhi ya wanafunzi tumewarudisha makwao baada ya kuona dalili ya
vurugu. Kuhusu adhabu kuna taratibu ambapo ni kuchapwa fimbo mbili
makalioni kwa wanaume na mikononi kwa wanawake. Nitajaribu kufuatilia
sakata hilo,” alisema Swai.
Note: Only a member of this blog may post a comment.