Ndanda Kosovo enzi za uhai wake.
MWIMBAJI nguli wa Muziki wa Dansi hapa
nchini kutokea Kongo, Ndanda Kosovo amefariki dunia leo Jumamosi asubuhi
katika Hospitali ya Taifa Muhimbili alikokuwa akitibiwa kwa maradhi ya
tumbo.
Akizungumza na Mwandishi wetu, Mmoja wa
Viongozi wa Wanamuziki wa Kongo chini Tanzania, King Dodoo amethibitisha
kutokea kwa msiba huo na kusema kuwa Ndandaa kosovo alifikishwa
Hospitali ya Mwananyamala juzi na kulazwa tatizo la maradhi ya tumbo.
Baada ya hali yake kuzidi kuwa mbaya, jana alihamishiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili ambako mauti yamemkuta leo asubuhi.
Ndanda Kosovo aliwahi kutamba na Bendi ya Wajelajela Original miaka ya 2000 na atakumbukwa kwa nyimbo kama, Jela, Chini Ya Uunzi, Chozi La Mnyonge na nyingine nyingi.
“NDANDAA KOSOVO APUMZIKE KWA AMANI!”
Note: Only a member of this blog may post a comment.