Sunday, April 3, 2016

Anonymous

Baada ya oparesheni 13 Millen Magese anapanga kuondoa kizazi, ushauri wa kwenda kwa TB Joshua je?

Mwanamitindo Mtanzania Millen Magese ambaye amekua akiishi na kufanya kazi Marekani amechukua likizo ya mwezi mmoja kufanya kampeni ya tatizo la kiafya ambalo limekua likimsumbua toka akiwa na umri wa miaka 13 na ikaja kugundulika akiwa na miaka 26 na mpaka sasa ameshafanyiwa Oparesheni 13 kutokana na tatizo la Endometriosis linalomkabili kwa maumivu kila anapokuwa kwenye mzunguko wake kama Mwanamke. 

Moja ya matokeo ya tatizo hili Millen anasema ni kusababisha kutopata mtoto na baada ya kuhangaika sana na kulipia gharama kubwa kwenye hospitali za Marekani na Afrika kusini, sasa amepanga kuoondoa kizazi mwezi April 2016 na hatua hiyo itasaidia afya yake kuwa na afadhali zaidi kuliko kipindi kilichopita. 

Anasema ‘sitakuwa naumwa kila mwezi, sitakuwa na mzunguko… Mungu akibariki nitaondoa kizazi April, hii sio mara ya kwanza kutaka kuondoa kizazi ni mara ya tatu, mara ya pili September 2015 nilifika kabisa mpaka natakiwa kuingia kusaini ili kitolewe lakini nikasema No siko tayari, huwezi kujua Mungu ana makusudi gani… atakaponiongoza nitakwenda ila siumii tena sababu kuna uwezo wa Mwanamke mwingine kunibebea mtoto wangu na nikaokoa maisha yangu kwa sababu nina mayai 

Kuhusu kwenda kuombewa kwa muhubiri maarufu wa Nigeria TB Joshua, Millen amesema ‘Sijakwenda kwa TB Joshua lakini ninachoamini hakuna mtu stong kuliko Mungu, imani yangu inaweza isiwe kwenye hayo Makanisa wanayoyatamka na mimi sio mtu wa kufata mkumbo, mimi ni Mkatoliki na nakwenda ninapotaka kwenda
Kumtazama Millen zaidi na kuelewa anayoyapitia unaweza kubonyeza play kwenye hii video hapa chini…
-via millardayo

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.