Friday, March 25, 2016

Anonymous

THEA Amkataa JOKATE KIDOTI Kwenye Uigizaji


IMG-20151118-WA0010-721x1024
Jokate Mwegelo.
Na hamida hassan
Msanii wa filamu wa ‘long time’ Bongo, Salome Urassa ‘Thea’ ameibuka na kusema kuwa yeye kama dairekta hamkubali Jokate Mwegelo kwenye suala zima la uigizaji wa filamu kwani anaamini kuwa bado ni cha mtoto.
Akipiga stori na Ijumaa kuhusiana na baadhi ya mamisi waliojiingiza kwenye uigizaji, Thea alisema wapo wengi ambao wamevamia fani huku akimtaja Jokate kama mmoja wao.
IMG_0651
Msanii wa filamu wa ‘long time’ Bongo, Salome Urassa ‘Thea’.
“Unajua zamani usingenishawishi kumdairekti Aunt Ezekiel kwani alikuwa hawezi kuigiza vizuri, sasa kidogo amekomaa baada ya kuigiza filamu nyingi ila Jokate bado anatakiwa kujifua kama kweli anataka awe kwenye listi ya waigizaji ninaowakubali,” alisema Thea. Jokate alipoulizwa kuhusiana na suala hilo, alichenga swali.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.