Rapper wa muziki wa Hip Hop, Stamina amekana kauli ya msanii mwenzake Chidi Benz, ambaye alisema kuwa Staa huyo kutoka Morogoro aliwahi kujiita jina lake.
Stamina ambaye kwa sasa ameachia album yake ‘Milima ya Uluguru’ amesema sijawahi kujiita jina la Chidi Benz kama mwenyewe anavyosema.
Stamina ambaye kwa sasa ameachia album yake ‘Milima ya Uluguru’ amesema sijawahi kujiita jina la Chidi Benz kama mwenyewe anavyosema.
Akiongea na Stori tatu ya Planet Bongo inayoruka kupitia EA Radio, Stamina amesema, “Sijawahi kujiita jina la Chidi Benz, kama yeye anasema aliwahi kuambiwa hivyo je, anaamini vipi hiko alichoambiwa. Ukiangalia staili zetu za kuchana ni tofauti kabisa labda ukimuangalia Fid Q utaona kuna chemistry inayofanana. Sina tatizo nae ndio maana hata kwenye wimbo wangu ‘Like A Father, Like A Son’ nimemshirikisha”
Chidi Benz alikiambia kipindi hicho kuwa, “Nimepata taarifa kuwa Stamina alikuwa anajiita jina langu la Chidi Benz, niliwahi kumwambia mwenyewe tulipokutana. Alipokuja mjini akasikia stori mbaya zangu akaacha kujiita jina hilo.”
CHANZO na Bongo5
CHANZO na Bongo5
Note: Only a member of this blog may post a comment.