Baba wa msanii wa filamu, Elizabeth Michael ‘Lulu’ Mzee Michael amezungumza jinsi alivyozipokea taarifa za kuwa mwanae alikuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi na marehemu Kanumba.
Muigizaji huyo mahiri bado anakabiliwa na kesi ya madai ya kumuua bila kukusudia aliyekuwa msanii wa filamu nchini, marehemu Steven Charles Kanumba.
Muigizaji huyo mahiri bado anakabiliwa na kesi ya madai ya kumuua bila kukusudia aliyekuwa msanii wa filamu nchini, marehemu Steven Charles Kanumba.
Akizungumza katika kipindi cha Take One cha Clouds TV Jumatano hii, Mzee Micheal amesema hakuamini kama kweli mtoto wake anaweza kutoka kimapenzi na Kanumba kwa kuwa wakati huo alikuwa chini ya miaka 16.
“Kwanza sikuamini kama Lulu anaweza, for this time alikuwa ana only 16 , alikuwa bado mdogo, alikuwa na miaka 16 na sikutegemea kabisa kama alikuwa ana uhusiano wowote labda wa mapenzi na nini katika umri huo,” alisema Mzee Micheal.

Aliongeza, “Lakini kama mzazi nilisikitika tu, nilisonononeka sana. Nimekuja nikawa namfuata kule mahakamani lakini hata kumuona siruhusiwi. Nilienda kule gerezani nimekuta kule alipokuwa anakaa, kwa kweli iliniuma sana. Lakini sikujua ile tukio kwanini lilichukuliwa kubwa sana, lakini baadae ilibidi tujipe moyo na muda umefanya haya yaliyotokea,”
Katika hatua nyingine Mzee Micheal amevitaka vyombo vya habari kutoa taarifa za ukweli ili kuepusha migongano ambayo inatokea kwenye jamii kwa kuandika habari bila kufuata miiko ya uandishi wa habari.
“Hii kitu labda ningeongea kwa waandishi wa habari, watoto wangu, ndugu zangu kwa sababu wapo wa age mbalimbali, hebu wajaribu kuandika vitu halisi vilivyotokea, kama ni tukio ni kweli liandike kama unatoa taarifa kama ilivyo.

Kwa sababu taarifa za uongo zinatuumiza sana, kama sisi wazazi tunaumia sana, hasa unavyokuta kile kitu nicha uongo. Mimi mara nyingi najikuta nachukua simu nampigia Lulu lakini Mama yake ana niambia hakuna kitu kama hicho. Kwa hiyo kwa jinsi wanavyoandika wanaweza hata wakatuletea maradhi,” alisema Mzee Micheal.
CHANZO na Bongo5
CHANZO na Bongo5
Note: Only a member of this blog may post a comment.