Staa wa Bongo Muvi, Shamsa Ford.
Showbiz
STAA wa Bongo Muvi,
Shamsa Ford kwa mara ya kwanza ameibuka na kuiongelea Ngoma ya Shika
Adabu Yako iliyoimbwa na Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ kuwa kamwe
hawezi kumhukumu Nay kwa maneno aliyoimba.
Shamsa Ford akiwa na Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’.
Akigonga mbili-tatu na Showbiz, Shamsa
aliyewahi kubamba na Filamu ya Chausiku alisema kuwa aliusikia wimbo
huo uliowachana mastaa wengi wa Bongo Muvi na kwamba bado hajajua
kinachomfaidisha Nay kupitia wimbo huo.
“Namuacha kama alivyo na kamwe siwezi kumhukumu kwa kile alichokiimba labda kwa upande wake aliona ni sawa,” alisema Shamsa.
Katika Wimbo wa Shika Adabu Yako, Nay
amewachana mastaa wa Muziki na Bongo Muvi ambao ni Shetta, Ommy Dimpoz,
Ray, Niva, Wema Sepetu na wengine wengi jambo lililosababisha Baraza la
Sanaa la Taifa (BASATA) kuufungia wimbo huo kutokana na ukiukwaji mkubwa
wa maadili, kashfa, uchochezi na kudhalilisha watu.

Note: Only a member of this blog may post a comment.