Tuesday, March 8, 2016

Anonymous

Serikali Yatoa Bei Elekezi ya Sukari..... Kilo moja Kuanzia sasa ni Sh. 1800 Nchi Nzima


HATIMAYE Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais John Magufuli imekisikia kilio cha muda mrefu cha Wananchi ambao walikuwa wakilalamika kupanda kwa bei ya sukari nchini.

Akizungumza na Waandishi wa Habari mchana huu jijini Dar es Salaam Mkurugenzi mkuu wa Bodi ya Sukari nchini,Henry Semwaza amesema kuanzia sasa kilo moja ya sukari itauzwa sh. 1800 nchi nzima.

"Serikali, kupitia bodi ya Sukari Tanzania, inawaarifu wananchi wote kuwa bei ya rejareja ya sukari sasa itakuwa sh. 1,800 kwa kilo moja. "Amesema Semwaza na kuongeza;

" Wafanyabiashara wote wanapaswa kuzingatia agizo hili, pamoja na kuhakikisha kuwa sukari inaendelea kusambazwa na kuuzwa kwa wananchi bila kuihodhi.

"Maafisa biashara wa mikoa na wilaya watafuatilia na kusimamia utekelezaji wa agizo kuhusu bei elekezi ya sukari, na hawatasita kuchukua hatua stahiki za kisheria kwa wale watakaobainika kupandisha bei ya bidhaa hiyo. "

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.