Saturday, March 12, 2016

Anonymous

NIYONZIMA Gumzo Kigali!

NIYONZIMA (7) Kiungo  wa Yanga, Haruna Niyonzima.
KIUNGO wa Yanga, Haruna Niyonzima amekuwa gumzo mjini hapa kutokana na kukubalika na mashabiki wengi wa soka jijini hapa.
Mashabiki hao walionekana kumfurahia Niyonzima kuliko nyota wengine wa kikosi hicho.
Yanga leo inacheza na APR mchezo wa raundi ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwenye Uwanja wa Amahoro.
Championi Jumamosi lilishuhudia mashabiki kibao wakilitaja jina la kiungo huyo na kudai kuwa Yanga nzima Niyonzima ndiye wanayempenda kwa kuwa pia ni Mnyarwanda mwenzao.
NIYONZIMANEW4Mashabiki wanaodhaniwa kuwa wa Rayon Sports timu pinzani na APR, walifika katika mazoezi ya Yanga na kumshangilia Niyonzima na nyota wengine wa Yanga.
Wakatio huohuo, shabiki mmoja wa Yanga ambaye ni Mtanzania jana alipata bahati ya kupiga ‘selfie’ za kutosha na mashabiki wa nchini hapa wakidhani ni kiungo wa timu hiyo, Thabani Kamusoko.

Shabiki huyo wa Yanga ambaye pia ana rasta kama Kamusoko, alipata shavu kufuatia kuzungukwa na mashabiki wenzake ambao ni raia wa Rwanda waliokuwa wakimpongeza kwa kazi nzuri anayoifanya katika kikosi hicho.
Licha ya shabiki huyo wa Yanga kutambua yeye siyo Kamusoko wala hakutaka kuweka wazi hilo zaidi alizidi kuonyesha manjonjo mbele ya Wanyarwanda hao ambao walionekana kuwa na mzuka wa ukweli wakidhani ni Kamusoko wa ukweli.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.