Na Gladness Mallya,RISASI mchanganyiko
DAR ES SALAAM: Kutokana na muda mrefu kutajwa kuwa ni mwanachama wa Freemason, staa wa Bongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ ameibuka na kusema kuwa hajawahi kujiunga ila kama kuna mtu anajua kama kweli kuna fedha yupo tayari kuunganishwa.

Akipiga stori na paparazzi wetu, Nay alisema mara nyingi amekuwa
akionyesha na kuzitumia alama za freemason kwa sababu anazipenda lakini
siyo kwamba ni mwanachama wao ila kama kuna mtu mwenye ufahamu vizuri
namna fedha zinavyopatikana huko, yupo tayari kuunganishwa kwani
anahitaji fedha zaidi.
Kwa upande mwingine Nay alisema sasa ameamua kubadili staili ya
maisha baada ya kupitia kwenye misukosuko mingi ikiwa ni pamoja na gari
lake kuvunjwa vioo na kutishiwa maisha kwenye simu na sehemu mbalimbali
anazopita.
“Namshukuru sana mama yangu kwani amekuwa akinipigia kelele kila
wakati kuhusu kubadili mwenendo wa maisha yangu, kwa mara ya kwanza
nimeenda kanisani baada ya kukaa kwa miaka kumi na moja bila kukanyaga
kwenye jengo hilo takatifu, hivyo naomba watu wasinifikirie vibaya,”
alisema Nay.
Note: Only a member of this blog may post a comment.