Thursday, March 10, 2016

Anonymous

Mwanadada PAM D Anaswa Live Kwa Dk. MWAKA

PAM-D-11.jpgPAM D (1) 
Msanii wa Bongo Fleva, Pamela Daffa ‘Pam D’ akitoka langoni kwa Tabibu JJ Mwaka.
Na mayasa Mariwata,
Dar es Salaam: Laivu! Kitengo cha Oparesheni Fichua Maovu (OFM) cha Global Publishers, kimemnasa msanii wa Bongo Fleva, Pamela Daffa ‘Pam D’ akizama kwenye Kliniki ya Tiba Asilia ya Fore Plan inayomilikiwa na Dk. Juma Mwaka ‘JJ Mwaka’ ambaye ni daktari bingwa wa masuala ya uzazi, ikidaiwa kuwa alikwenda kutafuta mtoto baada ya kushindwa kupata mimba kwa muda mrefu.
Tukio hilo lilijiri Ijumaa iliyopita kwenye kliniki hiyo iliyopo maeneo ya Ilala-Bungoni jijini Dar ambapo OFM iliweka kambi baada ya kung’atwa sikio na chanzo chake ambacho ni mtu wa karibu wa Pam D anayekimbiza na Ngoma ya Popo Lipopo.
Awali, OFM ilipokea ‘tipu’ kutoka kwa chanzo hicho kuwa, Pam D amekuwa akitimba kwenye kliniki hiyo mara kwa mara kwa lengo la kutaka kurekebisha mfumo wake wa uzazi kwani shida yake kubwa kwa sasa ni kunasa ujauzito.
PAM D (5) 
“OFM kwa taarifa yenu Pam D anasaga soli kwa Dk. Mwaka kila kukicha kwa sababu ana shida ya mtoto.
“Mimi ananishangaza sana kwa sababu bado ni binti mdogo lakini anahangaikia sana mtoto, mkitaka kuamini nendeni mkatege mingo pale kwa Dk. Mwaka leo (Ijumaa) mchana ana safari ya kwenda huko,” kilinyetisha chanzo hicho kwa sharti la kutochorwa jina gazetini.
PAM-D-11.jpg 
Baada ya kunyetishiwa ‘ubuyu’ huo, bila kupoteza muda, ‘kachero’ wa OFM alitinga eneo la tukio na kuweka mtego kwa masaa kadhaa ambapo ilipofika saa 8 na dakika kadhaa alasiri, bidada huyo alionekana akishuka kwenye Bajaj na kuingia kwa Dk. Mwaka.
Hakukaa muda mrefu kwani muda mfupi alitoka na kuingia kwenye Bajaj kisha kutimua eneo hilo.
Hata hivyo, kachero wetu alifanya ushushushu ndani ya kliniki hiyo kujua kilichompeleka Pam D lakini wahudumu wa Dk. Mwaka hawakutoa ushirikiano.
mwaka223Dk. Mwaka
Baadaye gazeti hili lilimtafuta Pam D kwa njia ya simu na kumuuliza kulikoni kutinga kwa Dk. Mwaka ambapo alionekana kushtushwa na mlolongo mzima wa ishu hiyo na kudai kuwa yeye ni binti mbichi hawezi kuhangaika na uzazi akiomba habari hiyo isiandikwe kwani wazazi wake hawatamuelewa.
“Ni kweli nilienda kwa Dk. Mwaka lakini ni kwa masuala yangu binafsi. Unajua kuna ishu nilikwenda kuzungumza naye kuhusu udhamini wa kazi yangu mpya ya muziki.
“Hayo mambo ya uzazi bado sijafikiria kuzaa, mkiandika hivyo mtanitafutia matatizo kwa wazazi wangu, ikaushieni,” alisema Pam D kwa unyonge.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.