Kanye West akiwa na mkewe Kim Kardashian.
HALI ni tete kwa wanafamilia, mwanamitindo na
mtangazaji, Kim Kardashian na rapa Kanye West baada ya tetesi kuendelea
kusambaa kuwa watoto waliowazaa pamoja, North na Saint siyo wa Kanye.
Tetesi hizo zilianza kuzagaa kupitia kipindi maarufu cha TV cha Maury
ambao taarifa zilielezwa kuwa Kanye West siyo baba halali wa North
West.
“Kuna ulazima wa kufanyika kwa DNA,” chanzo kilisema.
Napo, chanzo kingine kililitonya Jarida la Star;
“Wakapime DNA na kama ikigundulika Kanye hausiki nafikiri ni kumuacha Kim (Kardashian).”
Pia mtandao wa Hollywood Life ulilipoti kuwa Kim alitumia mbegu za mwanaume mwingine kwa ajili ya kuwapata North na Saint.
Duh! Endapo Kim atapigwa ‘kibuti’ atakuwa ameachika katika ndoa tatu
za halali. Ndoa ya kwanza alifunga na Damon Thomas na ya pili Kris
Humphries na baada ya hapo Kanye West.
(Imeandaliwa na Andrew Carlos/GPL)
Note: Only a member of this blog may post a comment.