Tuesday, March 29, 2016

Anonymous

MILIO YA RISASI YASIKIKA JENGO LA BUNGE

Kuna taarifa za milio ya risasi katika viunga vya jengo la Makao Makuu ya Bunge
la Congress, US Capitol Hill nchini Marekani.
Mashuhuda wanasema wameambiwa kwa vipaza sauti kuwa kila mtu ajifiche.

Taarifa za hivi punde zinasema mtu huyo mwenye silaha amekamatwa na polisi mmoja amepigwa risasi na kujeruhiwa.
Waandishi wa Habari waliokuwa kwenye eneo jengo la Bunge wameambiwa waendelea kubaki ndani.
Ikulu ya White House nayo imefungwa. Msemaji wa Polisi katika Jengo la Bunge hajasema lolote lakini ameahidi polisi kutoa taarifa za tukio hilo wakati wowote.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.