Friday, March 25, 2016

Anonymous

Ester Kiama wa Bongo Muvi Adaiwa Kufulia

Na Hamida Hassan
Staa wa filamu za Kibongo, Ester Kiama amedaiwa kufulia na ndiyo maana amekuwa haonekani kwenye viwanja vya kula bata kama ilivyokuwa kawaida yake.
Shosti wa karibu wa staa huyo aliyeomba jina lake lisitajwe alimwaga ubuyu kuwa, Ester kwa sasa anapitia kipindi kigumu cha kuchalala, ndiyo maana zile vurugu zake za mjini zimeisha.


“Kafulia ile mbaya, hata ile staili ya kubadili magari imekwisha, viwanja ndiyo haonekani kabisa,” alidai mtoa habari huyo.
Alipotafutwa Ester kujibu madai hayo alisema kwa kifupi: “Jamani sijafulia, maisha siyo kujirusha kila siku wala kubadili magari, nafanya mambo yangu yenye manufaa.”

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.