Wednesday, March 9, 2016

Anonymous

LYANGA: Tunashinda Mechi Zote Zilizobaki!


 
Danny Lyanga.
Ibrahim Mussa na Omary Mdose
BAADA ya wikiendi iliyopita Simba kukaa kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu Bara, straika wa timu hiyo, Danny Lyanga, ameibuka na kusema huu ni msimu wao na ana uhakika kwamba lazima watakuwa mabingwa, kwani wanataka kushinda mechi zote zilizobaki.

Simba iliyofikisha pointi 48 na kuziacha Yanga na Azam zikiwa na pointi 47, kabla ya mechi ya Yanga jana dhidi ya African Sports, wamebakisha mechi tisa kumaliza msimu huu na kama wakifanikiwa kuwa mabingwa watakuwa wamevunja mwiko wa misimu mitatu mfululizo.

Lyanga ambaye kwa sasa amekuwa akitumiwa zaidi na kocha wake, Jackson Mayanja, kama mchezaji wa akiba, amekuwa msaada mkubwa kikosini hapo kutokana na mara kwa mara kubadili sura ya mchezo kila anapopata nafasi hiyo.

Akizungumza na Championi Jumatano, mchezaji huyo alisema suala la yeye kuanzia benchi linatokana na mipango ya mwalimu kwa kuwa wanachokiangalia ni kuisaidia timu zaidi kuwa bingwa.
“Ni kweli nimekuwa nikianzia benchi, nadhani huu ni mkakati wa mwalimu mwenyewe wa nini anahitaji kwenye mchezo husika kwani lengo letu sote ni kuweza kuwa mabingwa msimu huu.

“Unajua kwa muda mrefu Simba imeshindwa kufikia malengo ikiwemo kuchukua ubingwa, lakini msimu huu ni mkakati ambao upo kwetu wachezaji kuhakikisha tunakuwa mabingwa kwa sababu ninaamini tunaweza kushinda mechi zote zilizobaki,” alisema Lyanga.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.