Maisha ya mastaa duniani hufuatiliwa kwa karibu sana na watu wengi.
Kuna kipindi yanakuwa ni asali lakini yanapobadilika huwa ni shubiri.
Mwanzo mahusiano ya Idris Sultani na Madam Wema Sepetu, yalionekana
kuvunjika lakini wenyewe wameonyesha kuwa bado wapo pamoja lakini
wameamua kuyaficha kwa sasa.
Akizungumza na kipindi cha Friday Night Live (FNL), kinachoruka
kupitia EATV, Idris alisema walifanya haraka kutangaza mimba ya Wema.
“Mwanzo tulifanya sana makosa kutangaza mimba ya Wema, culture yetu
hairuhusu. Tulitakiwa kuweka wazi kama ingekuwa mimba imefikia miezi
minne hivi na kuendelea,” alikiri.
Note: Only a member of this blog may post a comment.