Wachezaji wa klabu ya Manchester City Joe Hart na Raheem Sterling
watakosa mechi za kirafiki za England dhidi ya Germany na Holland baada
ya nyota hao wawili kuumia na kutolewa katika mchezo wao na Manchester
United.
Joe Hart aliumia mguu wake wa kulia katika harakati za kumuwahi
Anthony Martial asifunge baada ya pasi mbovu ya nyuma kutoka kwa beki
Martin Demichelis na Sterling alitolewa kipindi cha kwanza baada ya
kugongana na Juan Mata.
Kwa mujibu wa kocha wa City, Manuel Pellegrini amesema nyota hao
watakuwa nje kwa mwezi mmoja na kukosa mechi za maandalizi ya Timu ya
Taifa kwa ajili ya Euro 2016, ambapo England itajipima nguvu na Ujerumani
huko Berlin Jumamosi ijayo kabla ya kurejea Wembley kuikabili Holland
siku tatu baadae.
Note: Only a member of this blog may post a comment.