Tuzo za muziki wa Afrika za Kora zilizokuwa zifanyike Jumapili, March
20 jijini Windhoek, Namibia, zimeahirishwa baada ya kampuni iliyopewa
kazi ya kuandaa jukwaa na utayarishaji kushindwa kupata vifaa
vinavyotakiwa katika muda muafaka.
Katika maelezo yake, waandaji wa tuzo hizo wamedai kuwa bado wanaendelea kuweka sawa mipangilio ya ukumbi, hoteli za kuwaweka wageni kutoka nchi mbalimbali pamoja na kumalizia kukusanya fedha za udhamini kuwezesha tuzo hizo.
Maelezo hayo yamedai kuwa baadhi ya vifaa vilikuwa visafirishwe kutoka nchini Afrika Kusini.
“Bahati mbaya, licha ya jitihada zetu, hadi leo hatujapokea ruhusa ya kuliwezesha kampuni husika kuingiza vifaa nchini Namibia kwaajili ya March 20, siku ya tuzo,” yalisema maelezo ya kampuni ya,” Mundial Telecom Sarl waandaji wa tuzo hizo.
Imeomba radhi kwa kuahirishwa kwake na imesema itatangaza tarehe mpya.
Tuzo hizo zimekuwa na matatizo mengi awali ikiwa pamoja na baadhi ya show kusitishwa kabisa, washindi kushindwa kulipwa na watumbuizaji kuingia mitini.
Diamond, Vanessa Mdee, Wakazi, Yamoto Band na Mrisho Mpoto wametajwa kuwania tuzo hizo mwaka huu.

-via bongo5
Note: Only a member of this blog may post a comment.