Bado headlines za makocha wa vilabu vya Ligi Kuu Uingereza zinazidi kushika kasi katika vyombo vya habari vya Uingereza, kocha wa Man United Louis van Gaal na aliyekuwa kocha wa Chelsea Jose Mourinho ndio walikuwa wanaongoza kwa kuandikwa.
March 15 headlines zimeahamia kwa kocha wa klabu ya Arsenal Arsene Wenger, ambae weekend iliyomalizika klabu yake imeondolewa katika michuano ya Kombe la FA, wiki iliyopita kwenye mchezo dhidi ya Hull City shabiki wa Arsenal alionekana akionesha bango linaloshinikiza ajiuzulu.
Kama hiyo haitoshi March 15 pia kuna tetesi zimeandikwa na mtandao wametro.co.uk kuwa mashabiki wa Arsenal wanataka Wenger aondoke na nafasi yake irithiwe na Diego Simeone au Manuel Pellegrini.
Mtandao wa dailymail.co.uk wenyewe ndio umeandika kuwa Wenger ataondokaArsenal kama mashabiki wa Arsenal wakiendelea kutokuwa na imani nae.
Kutoka kushoto ni Diego Simeone, Wenger na Pellegrini

Note: Only a member of this blog may post a comment.