Wednesday, March 9, 2016

Anonymous

Baba LEVO Kafunguka Kuhusu Kuishi Kwa SHILOLE na Kutumia Gari Yake....

Baba Level ameweka bayana mambo yote hayo alipokuwa akifanya mahojiano katika kipindi cha E News kinachorushwa na kituo cha EATV.
”Mimi nimeanza kupanga jijini Dar es salaam mwaka 1999 kipindi ambacho Shilole alikuwa zake huko Igunga mkoani Tabora ambapo sasa mimi ni baba wa familia nina mke na watoto hivyo stori kama za kuambiwa natumia gari ya Shilole labda kama kuna mtu anasema hivyo ili kupata umaarufu”-Amesema Baba Levo

”Suala la mimi kuhusishwa na mambo ya Shilole tena kuomba gari ni kunichafua na watu lazima wajue kwenye siasa nilichafuliwa vya kutosha na bado nikawashinda”-Amesisitiza Baba Levo.
Aidha msanii huyo kwa sasa ni Diwani wa kata ya Mwanga Kigoma mjini kupitia ACT Wazalendo ambapo alichaguliwa katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.