Tukio hilo lilitokea tarehe 27/02/2016 majira saa 1:45 jioni katika kituo cha polisi Lugulu wilaya ya Itilima Mkoani hapa, ambapo askari huyo alikuwa akifanyia kazi.
Kamanda wa polisi Mkoani hapa Onesmo Lyanga akitoa taarifa kwa waandishi wa habari jana, alisema kuwa mtuhumiwa aliyetoroshwa na askari huyo alikuwa akikabiliwa na kesi ya mauaji namba ITL/IR/95/2016 ambaye ni Mkulima wa kijiji cha Gambasingu.
Lyanga alisema kuwa askari huyo amefukuzwa kazi kwa fedheha, ambapo mbali na hatu hizo atafikishwa mahakamani kwa makosa ya jinai.
Aidha Kamanda Lyanga alisema kuwa mbali na askari huyo kuchukuliwa hatua hizo, jeshi hilo linawashikilia jumla ya watu wanne kwa kuhusika na utoroshwaji wa mtuhumiwa huyo.
Aliwataja watu hao kuwa ni Juma Zakaria (40) mkazi wa kijiji cha Budalabujiga, Agnes Nzige (40) mkazi wa kijiji cha Gambasingu, Malika Kilindila (16) mkazi wa kijiji cha Gambasingu, pamoja na Robert Mandagani (62) ambaye ni mkazi wa kijiji cha Inalo.
Katika hatua nyingine Kamanda huyo alisema kuwa amefanya mabadiliko katika kikosi cha askari wa usalama barabarani, kwa kuwaondoka askari nane (8) kutokana na kukiuka maadili ya jeshi hilo.
Lyanga hakuweza kuwataja askari hao, ambapo alieleza uchunguzi dhidi yao unaendelea huku wakiwa wamehamishiwa katika vitengo vingine vya jeshi hilo.
Note: Only a member of this blog may post a comment.