Monday, March 7, 2016

Anonymous

3 PICHAZ: Diamond Platnumz Marekani Akiwa na Ne-Yo na Mwigizaji wa Series ya EMPIRE


Kwenye OnAIR with Millard Ayo Diamond Platnumz alisema March 2016 anakwenda Marekani na kwamba atafanya kazi kubwa na nyingi ikiwemo video ya kolabo yake na staa wa muziki duniani Ne-yo ambaye makazi yake ni Marekani……. so inaonekana Diamond anatimiza alichokisema.

Moja ya vitu alivyoongea kwenye hiyo Exclusive Interview ni pamoja pia na kukutana na Producer maarufu Swizz Beatz ambaye mikono yake imefanya kazi na mastaa kibao akiwemo Jay Z ambapo D alisema atarekodi pia na alikua anaangalia uwezekano wa kufanya kumshirikisha Alicia Keys pia ambaye ni mke wa Swizz Beatz.

Diamond na Yazz

Sasa kwenye hii post nimekuwekea picha tatu alizopiga na mastaa tofauti wa Marekani akiwemo Rapper Kanye West, mwigizaji Yazz kutoka kwenye series ya EMPIRE pamoja na mwimbaji Ne-yo ambaye walirekodi wimbo pamoja Nairobi mwishoni mwa mwaka jana.

Yazz

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.