Issue ya uhaba wa sukari ilichukua headline baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania John Pombe Magufuli kupiga marufuku uingizaji wa sukari kutoka mataifa ya kigeni ili kuvilinda viwanda vya sukari nchini ambavyo vimeathiriwa na uingizaji na uagizaji wa sukari ya bei rahisi kutoka nje.
Kuzuiwa kwa sukari ya nje ikasemekana kumesababisha tatizo la mfumuko wa bei ya sukari licha ya kuzalishwa kwa wingi hapa nchini. Leo March 7 2016 Waziri wa Viwanda na Biashara Charles Mwijage amezungumzia hilo wakati akijibu maswali ya wanahabari na kukanusha kuwepo kwa uhaba wa sukari nchini….
>>> ‘Hakuna uhaba wa sukari, kuna
sukari ya kutosha na ambaye anaficha hiyo sukari yake kwanza
nimeshaagiza tena nije nimtafute mkurugenzi wa leseni kama kuna godown
lina leseni nikalifunge godown tuone huyo anayeficha sukari‘:-Charles Mwijage
>>>’kwa
hiyo hakuna uhaba wa sukari kama kuna mtu anajua kuna mtu anaficha
sukari aje aniambie, mimi naweza kufunga godown la mtu yeyote hapa
nchini simuogopi mtu yeyote kwa hiyo hakuna uhaba, uhaba unatengenezwa,
mimi nafanya survey nauliza sukari inauzwa bei gani kwenye maeneo
mbalimbali nchini‘:-Charles Mwijage
Awali Waziri huyo amezungumzia ujio wa Rais wa Vietnam, Truong Tan Sang,
huku akibainisha umuhimu wa ujio wa Rais huyo hasa katika kuchochea
mageuzi ya kiuchumi na maendeleo ya watu, Waziri Mwijage ameelezea lengo
la ujio huo…
‘tujifunze
kwa hawa watu ambao walikuwa kama sisi, lakini sasa hivi wako mbali
sana, ukiangalia takwimu zetu za biashara, tofauti ya kiasi tunachoagiza
kwao na tunachonunua tuna tofauti ya dola milioni 49, lakini tunapenda
washirika wetu hawa wanunue zaidi kwetu na sisi tununue zaidi kwao
lakini zaidi ni namna wanavyofanya kazi‘:-Charles Mwijage
Note: Only a member of this blog may post a comment.