Monday, February 29, 2016

Anonymous

Walimu Hawakupaswa Kupanda Daladala Bure Huu ni Udhalilishaji Mkubwa

Najua kuna watakaonipinga, nakubaliana nao kutokukubalina. Nimeliona hili jana kwenye vyombo vya habari. Wengine watashangilia lakini kwenye utekelezaji litaleta msuguano mkubwa sana. Tujiulize huu ndo msaada wanaotaka walimu? Badala ya kuwapatia posho? Mnadhani kadhia ya kunyanyaswa watakayoipata kwenye daladala kutoka kwa makondakta ni ndogo?Nambie kondakta atakapogundua amepakiza walimu watano kwenye daladala wamekaa na wanafunzi kadhaa huku kuna abiria wengine wamebak. 

Unadhan huyu konda atasema nini? Mtasababisha usafiri kuwa mgumu kwa walimu. Maana daladala zitakuwa hazitak kusimama sehemu zenye vituo vilivyo karibu na shule kwa kuhofia kubeba walimu' hasara' unadhani kondakta akipunguza 10,000 katika marejesho yake kwa siku kwa tajiri akamwambia alibeba walimu. Tajiri atamwelewa? Kweli nawaambia walimu watadhalilishwa sana na tutegemee kusikia wakiambiwa waachie siti ili wakae wenye kulipa nauli. Tutegemee majina mengi ya manyanyaso . tutegemee wakidhalilishwa sana kutokana na jambo hili. Mimi ninheshauri waongezewe posho. wapewe posho ya nauli huu ndo ulikuwa ufumbuzi. Hapa ilikuwa ni kuwaheshimu.
Kuwaambia wapande daladala bure ni kuwanyanyasa, kuwadhalilisha. Tena kuwapatia vitambulisho maalum ni kuwafanya wawe watu maalum ambao jamii imewafanya siku zote waishi kwa huruma. Ni aibu mwalimu anapokaa na wenzake hata sehemu ya starehe anaambiwa asitoe pesa anywe ale bure na wenzie kwa kuwa wanajua yeye ni mwalimu mshahara wake mdogo. Na hili si jambo la furaha au faraja. Ni udhalilishaji. Tunakoenda kutakuwa na michango maalum ya walimu kwenye harusi na pengine nako wakaambiwa wawe wanahudhuria bure. Walimu hawahitaji kupanda daladala hata ndege bure. Wanataka wawezeshwe kulipia kama wengine. Ni hayo tu
-by Sodoku

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.