Tuesday, February 23, 2016

Anonymous

VIDEO+PICHAZ: Shuhudia Rais MAGUFULI Alivyokutana na Balozi wa Uingereza Ikulu!

Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, Diana Patricia Melrose amekutana na Rais Magufuli ili kufikisha ujumbe maalum wa pongezi kutoka kwa Waziri Mkuu wa Uingereza, David Cameron kutokana na utendaji wake uliotukuka na nawa vitendo katika kukusanya mapato ya serikali, kupambana na rushwa/ufisadi, ubadhilifu wa mali za umma na uzembe.

Balozi Melrose amesema Waziri Mkuu Cameron amevutiwa sana na utendaji wa Rais Magufuli na kusisitiza kwamba Nchi hiyo itaendeleza ushirikiano wa karibu uliopo kati ya Uingereza na Tanzania ili ndoto za Watanzania kimaendeleo zitimie.
''Waziri Mkuu, Cameron amesema yuko tayari kushirikiana kwa karibu na serikali yako katika eneo la inteligensia na pia kuziwezesha mahakama zifanye kazi kwa ufanisi zaidi'' Alisema Melrose.
PICHA:

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Balozi wa Uingereza hapa nchini, Bi. Dianna Melrose, Ikulu jijini Dar es Salaam

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa, Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Balozi wa Uingereza hapa nchini, Bi. Dianna Melrose. 

Bonyeza play au download kutazama video hiyo hapa chini;

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.