Tuesday, February 23, 2016

Anonymous

Kuelekea Mechi ya ARSENAL Vs FC BARCELONA, Luis SUAREZ Kafanya Kituko Hiki na Kuwashangaza Mashabiki wa Soka Duniani...


Mshambuliaji wa kimataifa wa Uruguay ambae amewahi kuichezea klabu ya Liverpool ya Uingereza na baadae kujiunga na klabu ya FC Barcelona ya Hispania Luis Suarez amewashangaza wengi baada ya kuingia kwenye headlines saa chache kabla ya kusafiri kwenda London Uingereza kwa ajili ya mechi dhidi ya Arsenal. 

Suarez ambae huwa anaingia kwenye headlines kwa kesi zake za kujiangusha uwanjani na kung’ata wachezaji wenzake uwanjani, alishangaza wengi baada ya kujulikana kuwa kasahau passport yake kwao Uruguay ambayo ndio anatakiwa kuitumia kusafiria kwenda London katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Arsenal.
download
Hata hivyo baada ya kujulikana kuwa amesahau passport, mmoja kati ya watu kutoka katika uongozi wa FC Barcelona aliifuata passport hiyo Uruguay. Luis Suareiz akishirikiana na Neymar na Lionel Messi kwa pamoja wamefunga jumla ya goli 91 msimu huu, wakati Suarez pekee amefunga jumla ya goli 41.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.