Beki wa Simba, Abdi Banda.
Said Ally, Dar es Salaam
UONGOZI wa Simba umeliandikia barua Shirikisho la Soka
Tanzania (TFF), kupinga kadi nyekundu aliyoonyeshwa beki wao, Abdi
Banda, katika mchezo dhidi ya Yanga wiki iliyopita.Banda alionyeshwa kadi nyekundu na mwamuzi Jonesia Rukyaa katika mchezo wa watani wa jadi, katika dakika ya 25 baada ya kumchezea vibaya straika wa Yanga, Donald Ngoma raia wa Zimbabwe.
Akizungumza na Championi Jumatano, Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara, alisema wameshaiandikia barua TFF na jana Jumanne waliiwasilisha kwa shirikisho hilo, hivyo wanasubiri majibu.
Alisema kikubwa kilichowasukuma kufikia uamuzi huo ni kutokana na mazingira ya jinsi tukio lilivyotokea na mchezaji wao kupewa kadi nyekundu inaonyesha wazi kuwa mwamuzi hakuwa sahihi.
“Tunaamini kuwa TFF watatenda haki kwenye jambo hili,” alisema Manara.

Note: Only a member of this blog may post a comment.