Beki wa pembeni wa Simba, Hassan Kessy.
Wilbert Molandi, Dar es Salaam
BEKI wa pembeni wa Simba, Hassan Kessy, wikiendi iliyopita aliimaliza vibaya baada ya kupokea simu nyingi za mikwara na vitisho akilaumiwa kutokana na kuifungisha timu hiyo ilipovaana na Yanga.
BEKI wa pembeni wa Simba, Hassan Kessy, wikiendi iliyopita aliimaliza vibaya baada ya kupokea simu nyingi za mikwara na vitisho akilaumiwa kutokana na kuifungisha timu hiyo ilipovaana na Yanga.
Katika mechi hiyo iliyomalizika kwa Yanga kushinda mabao 2-0, beki huyo
alisababisha bao la kwanza dhidi ya timu yake, baada ya kumrudishia pasi
fupi kipa wake, Muivory Coast, Vincent Angban ambayo ilinaswa na Donald
Ngoma na kufunga katika dakika ya 39.
Hassan Kessy akifanya maombi.
Kosa hilo, lilionekana kuwakera mashabiki wa Simba waliokuwepo
uwanjani hapo na kumtolea lawama beki huyo ambaye alikuwa ameonyesha
kiwango kizuri kwenye michezo saba iliyopita.
Akizungumza na Championi Jumatano, Kessy alisema kuwa tangu mechi hiyo ya Yanga imalizike, anapata usumbufu mkubwa kutoka kwa mashabiki ambao kila wakati wanampigia simu na kumtumia meseji za mikwara na vitisho.

Kessy alisema, anashangaa kuona mashabiki hao wakiendelea kumpigia simu
na kumtumia meseji, licha ya kuwaomba msamaha kwa makosa hayo
aliyoyafanya.
Aliongeza kuwa, kikubwa anachokifanya yeye hivi sasa ni kukaa kimya
ili kuepusha matatizo mengine kwa faida yake na badala yake anaendelea
kutimiza majukumu yake ya ndani ya uwanja akiwa na Simba.
“Mchezo wa soka ni wa uvumilivu sana na hadi hapa nilipofikia kukaa
kimya kugombana na shabiki yeyote nimejitahidi kutokana na simu
ninazopigiwa na meseji ninazotumiwa na mashabiki wa Simba.
“Wengi wao wanaonipigia simu na kunitumia meseji, wanalalamika kuwa mimi nimesababisha tufungwe baada ya kufanya kosa la kurudisha pasi fupi kwa kipa kabla ya Ngoma kufunga.
“Wengi wao wanaonipigia simu na kunitumia meseji, wanalalamika kuwa mimi nimesababisha tufungwe baada ya kufanya kosa la kurudisha pasi fupi kwa kipa kabla ya Ngoma kufunga.
“Kikubwa wanachotakiwa kukifahamu ni kuwa, soka ni mchezo wa makosa
ambayo mimi niliyafanya na kusababisha tufungwe bao moja katika kipindi
cha kwanza, ninaomba nichukue nafasi hii kuwaomba radhi Wanasimba wote,”
alisema Kessy.
Aidha, alipotafutwa meneja wa mchezaji wa timu hiyo, Athumani Tippo
kuzungumzia suala hilo, kwanza kabisa alikiri kuwepo na taarifa hizo za
mchezaji wake kutishiwa maisha na mashabiki wa Simba
“Hizo taarifa za kweli kabisa, mchezaji wangu wanamtumia meseji na
kumpigia simu za vitisho, hivyo hivi sasa nimepanga kukutana na
mwanasheria wangu ili kuhakikisha sheria inachukua mkondo wake,” alisema
Tippo.

Note: Only a member of this blog may post a comment.