Dar es Salaam:
‘Uswahilini’ kuna msemo kwamba, mwanaume au kijana rijali ni yule mwenye
rekodi ya kutoka kimapenzi na wasichana wengi lakini mimi nakataa!
Kama ni kweli basi ilikuwa zama za kale
lakini siyo zama hizi za vifo na magonjwa. Hakuna mwanaume rijali wala
kidume, bali staha ndiyo nguzo ya kila mmoja.
NAMUUNGANISHA DIAMOND
Makala yangu ya leo nimeguswa sana kumzungumzia Mbongo Fleva, Nasibu Abdul almaarufu Diamond.
Kumekuwa na habari kwenye vyombo mbalimbali vya habari, hususan magazeti kumhusu Diamond.
Licha ya uwezo wake mkubwa kwenye muziki wa kizazi kipya, dogo ni sukari ya warembo kwa maana ni maarufu kwa kubadili wanawake.
HAPA NDIPO PENYE HATARI
Napenda kutumia makala haya kumwambia
Diamond kuwa, umri wake ukilinganisha na idadi ya warembo aliotoka nao
haviendani kiasi kwamba, nikijaribu kumpigia mahesabu napata shida
kuamini.
Diamond kwa sasa ana miaka 26. Ina maana
kama uwezo wa kuanza kumudu kuwa na wanawake kama rijali, ni pale
alipokuwa na miaka 18. Ukichukua 26 -18= 8.
Ina maana kwamba, Diamond kwa muda wa
miaka 8 amekuwa na mzunguko mkubwa wa mademu. Mtungo wake unaonesha staa
huyu ameshatoka na warembo 14!! Hapo achilia mbali wale ambao ilikuwa
siri yake na hawakuwahi kuandikwa magazetini.
Kwa hiyo kwa hesabu za haraka, Diamond
amekuwa na demu mmoja kila baada ya miezi kama kumi tu. Huo ni wastani
wa jumla, hata kama kuna wengine alidumu nao kwa miaka miwili na wengine
miezi mitatu.
KIAFYA IMEKAAJE?
Kila nikimfikiria Diamond, napata tabu
kwani naamini umri wake (miaka 26) ni mdogo sana kwa kuwa na mzunguko
mrefu kiasi hiki. Mbaya zaidi ni mzunguko wenye mizunguko ambayo nayo
pia ina mizunguko. Sitaki kumchambua ila ukiangalia picha inajionesha
kila kitu!
Niliwahi kuongea na mtaalam mmoja kuhusu
afya ya mwanadamu, hasa katika umri mdogo na ngono! Mtaalam huyo
aliniambia kwamba, uhusiano wa wapenzi wengi katika ujana unaweza kuwa
na madhara mengine ya kivionjo yanayoweza kubadilisha mahusiano mazuri
kuwa mabaya.
KINACHOONEKANA KWA DIAMOND
Mtaalam huyo alisema kijana anayependa
kufanya tendo la ndoa mara kwa mara hujikuta akikosa msisimko haraka
sana. Na hali hii humfanya asidumu katika uhusiano kwa muda mrefu na
kuanzisha mpya kwa sababu ya kupoteza msisimko na yule wa awali.
MWILI KUTAWALIWA NA TAMAA

“Lakini pia tabia ya kufanya mapenzi
mara kwa mara katika umri wa ujana huongeza uzalishaji wa homoni mwilini
na kuufanya uwe na msukumo mkubwa wa kutaka kuridhishwa kwa tendo la
ndoa bila kukosa na hivyo humfanya mhusika awe mtumwa wa ngono,” alisema
mtaalam huyo.
HAPA KWENYE MAGONJWA SASA
Wanaofanya mapenzi holela mara kwa mara huwa katika hatari kubwa ya kuambukizwa magonjwa ya zinaa.
Kama Diamond hayupo makini (kwa
kutotumia zana, lakini naamini ni makini) ina maana kwamba, anaweza yeye
kuambukizwa au kuambukiza. Kama mrembo wake X alikuwa ana ugonjwa
akampa yeye wakati huohuo akaachana naye, yeye akaanza uhusiano na
mrembo Y, atampa ugonjwa ambao naye atausambaza tena na tena.
Hii ndiyo hatari ninayoiona kwa Diamond. Kwa hapa namsisitizia kuwa makini na kujichunga sana.


Note: Only a member of this blog may post a comment.