ALIYEKUWA
mchumba wa staa wa Bongo Muvi, Jacqueline Wolper, Ramadhan Mtoro
‘Dallas’ inadaiwa kuwa hivi karibuni amefunga ndoa na mwanamke mmoja
aliyefahamika kwa jina la Suleiya, Amani lina mchongo kamili.
Kwa mujibu wa chanzo chetu, tukio hilo
lilijiri Jumapili iliyopita maeneo ya Mbezi-Ununio jijini Dar ambapo
wawili hao walionekana wakiwa katika hali ya furaha muda wote huku ndoa
hiyo ikifungwa bila kificho.
“Hatimaye leo yamekuwa, yaani yule jamaa
(Dallas) aliyekuwa akimpatia Wolper magari ya kifahari na mipesa leo
hii saa saba mchana (Jumapili) anafunga ndoa tena na mwanamke mwingine
mkali kuliko hata huyo Wolper,” kilisema chanzo.
Baada ya kuunyaka ubuyu huo, Amani lilifanikiwa
kutimba eneo la tukio na kushuhudia Dallas akifunga ndoa kweli na
mwanamke huyo ambapo baadaye waliingia moja kwa moja kwenye gari na
kutokomea.
Miaka mitatu iliyopita Dallas alikuwa
katika uhusiano wa kimapenzi na Wolper hadi kufikia hatua bi’dada huyo
kubadili dini ili aolewe naye lakini mwishowe uhusiano huo uliyeyuka.

Note: Only a member of this blog may post a comment.