Thursday, February 25, 2016

Anonymous

Donald TRUMP Azidi Kupeta Mchujo wa Kugombea Kiti Cha Urais Marekani

Mgombea urais wa Chama cha Republican, Donald Trump ameshinda katika Jimbo la Nevada nchini Marekani, na kuzidi kuimarisha uongozi wake katika mchujo wa kuwania tiketi ya chama hicho.

Tajiri huyo aliyewahi kutamka hadharani kuwa atawafunga jela Rais Mugabe na Museveni, sasa ameshinda mara tatu, kufuatia ushindi wake katika Jimbo la New Hampshire na Carolina Kusini.
Seneta Marco Rubio na Ted Cruz ambao wamekuwa wakishambuliana wiki hii wanapigania nafasi ya pili.
Maofisa wa chama hicho wamesema wanachunguza ripoti za watu kupiga kura mara mbili huku eneo moja likidaiwa kuwa na vifaa vichache vya kupigia kura.
Baadhi ya wapiga kura pia walidaiwa kuvaa nguo zenye picha za Trump, lakini maofisa wamesema kuwa hatua hiyo siyo kinyume na sheria

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.