Na Gladness Mallya
WAKATI mamia ya wakazi wa Dar es
Salaam waishio mabondeni na pembezoni mwa bahari na mito wakihaha
nyumba zao kuvunjwa, staa wa filamu Bongo, Rose Ndauka amesema hajali
kama nyumba yao itakutwa na bomoabomoa hiyo.
Badala yake, alimpongeza Rais John
Magufuli kwa kusimamia zoezi hilo, kwani wengi wa wanaobomolewa
walishapewa taarifa mapema na hawakutii agizo hilo la serikali, lakini
akaitaka kuwaangalia kwa jicho la tatu watu ambao hawakupewa taarifa za
zoezi hilo.
“Wazazi wangu wakibomolewa nyumba naona
kawaida tu, siwezi kuwa na presha maana kila kitu kinapangwa na Mungu,
kama ni kubomoa wabomoe tu hatuna la kufanya,” alisema Rose.

Note: Only a member of this blog may post a comment.