Hivi unaanzaje kuleta mzaha na nyoka mtu wangu ?! Eti nyoka unamuiba na bado unamficha kwenye nguo ya ndani uliyovaa ???
Mama mmiliki wa duka linalouza nyoka pamoja na wadudu wengine la A to Z Pets lililopo Portland, Oregon Marekani
analalamika tu kitendo cha jamaa huyo aliyeingia kama anachekicheki
hivi ahudumiwe alafu akatoka na nyoka aliyemuiba na kumficha kwenye nguo
ya ndani aliyovaa.
Mama huyo Christin Bjugan
amelalamika kwamba nyoka wao mwenye thamani ya kama dola 200 hivi
kaibiwa na jamaa huyo, kilichosaidia akamgundua mwizi wake ni camera za
CCTV alizozitega ndani ya duka lake.
Unaweza kuona tukio lote lililonaswa na CCTV mpaka jamaa anapoiba nyoka kwa kumuingiza kwenye nguo ya ndani kwenye hii video hapa.
Note: Only a member of this blog may post a comment.