Wapendwa wanajukwaa na watanzania kwa ujumla, ni dhahiri kwamba sote tunapenda kuona nchi yetu ikisonga mbele kitaifa na kimataifa katika michezo na sanaa mbalimbali. Tumeshuhudia baadhi ya vijana wetu wakifanya vinzuri kimataifa na kuiletea heshima tele nchi yetu.
Sasa pamoja na heshima hii nina jambo ambalo naliona hakika halijakaa sawa na pengine linaleta picha mbaya kwa wananchi kuanza kudhani labda ni michezo au sanaa za aina fulani tu ndizo ambazo serikali inazithamini. Ni wiki iliyopita ambapo tumeshuhudia mchezaji wa soka Mbwana Samatta akitangazwa kuwa mchezaji bora wa Afrika kwa wachezaji wanaocheza ndani ya Afrika. Tumeshuhudia namna serikali ilivyomtembeza mtaani kama kumpongeza kwa tuzo aliyopata. Leo hii muda huu Vodacom na serikali wameandaa hafla ya kumpongeza kwenye Hotel ya Hyat Regend. Kwa mujibu wa posts zinazowekwa na Vodacom katika mtandao wa instagram ni kwamba Samatta amepewa zawadi na serikali pesa taslim na kiwanja huko Kigamboni. Napongeza kwa hilo ni jambo jema hasa katika kutia moyo.
Pamoja na mafanikio yote hayo hakuna hata kiongozi mmoja aliyediriki kumpa hongera Diamond kwa tunzo kubwa ya Dunia aliyoipata. Nimejiuliza sana na kudhani labda michezo na sanaa zinazothaminika na serikali ni mpira wa miguu tu.
Note: Only a member of this blog may post a comment.