Tuesday, January 12, 2016

Anonymous

Ndoa Yangu Hatarini, Napewa Unyumba Kwa Kulazimisha!

Wadau,
Nimeoa kama miaka mitatu iliopita tatizo nalotoka tubadilishane mawazo ni mwenza wangu mke kuanzia mwaka jana amekua akinipa unyumba kwa mbinde kweli.Naweza fukuzia wiki nzima nikawa napewa jibu nimechoka nimechoka, siku nikilazimisha anasema fanya basi, nibake sasa na mimi nakua nahamu nafanya bila ushirikiano wowote kama vile nafanya na maiti, lakini kutokana na ukame wakati mwingine namuacha chumbani na kwenda kufanya mastabesheni sebuleni.

Nimejaribu kila namna kujua tatizo nimeshindwa wakati mwingine shetani ananiingia nitafute mchepuko wa kukataa kiu yangu ila moyo mzito nampenda mke wangu lakini pia madhara ya kuchepuka mengi. Nimejitahidi kufwatilia kama kapata mtu mwingine hakuna ushahidi kwa hilo pengine anaridhishwa sijapata dalili hizo. Nimejitathimini kama nilimkosea hakuna hivyo nimeleta hapa mnisadie wadau kunusuru ndoa yangu.

Maana kunyimwa tendo la ndoa bila sababu maalumu napata wakati mgumu msaada kwa wakubwa humu.
Tatizo nini...tubadilishane uzoefu...
Salaam...wote inauma saana kutongoza wife ndani ya ndoa ili upate mzigo.



 -By Juma

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.