Soka ni mchezo unaopendwa sana duniani
ila uzuri wa mchezo huu ili uweze kukuvutia ni pale wachezaji
wanapocheza kwa ushirikiano wa kupeana pasi za mwisho za kifundi na
mshambuliaji kufunga goli, kitu ambacho kinaongeza mvuto zaidi kwa
mashabiki kufurahia soka.
Najua unajua headlines za kiungo wa kimataifa wa Ujeruamani anayekipiga katika klabu ya Arsenal ya Uingereza Mesut Ozil kuwa moja kati ya wachezaji mahiri wanaoongoza kutoa assist za magoli katika soka, lakini Ozil bado anashikilia rekodi ya kuongoza kumpa pasi za mwisho Cristiano Ronaldo na kufunga magoli.
Ozil pia ndio mchezaji wa Arsenal anayeongoza kwa kutoa assist nyingi zaidi ila leo December 3 ikiwa ni siku ambayo wengi wetu tunaitumia kupost TBT
Pichaz katika mitandao ya kijamii, naomba nikusogezee Top 20 ya assist
kali zaidi katika historia ya soka, miongo mwa waliong’aa ni Zlatan Ibrahimovic wa PSG, Xabi Alonso, Andre Pirlo na mastaa wengine wengi.
Unaweza cheki video ya dakika 10 ikikuonesha Top 20 video ya assist kali
Note: Only a member of this blog may post a comment.