Na Mwandishi Wetu
Mara tu baada ya uzinduzi wa kampeni jijini Dar es Salaam, mgombea wa urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Pombe Magufuli ‘JM’ kwa sasa anazidi kutikisa mikoani.
Magufuli alianzia mkoani Katavi ambako alipata mapokezi ya mafuriko kabla ya kuelekea Rukwa akiwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda ambao kwa pamoja walikusanya umati mkubwa kila walikopita.
Katika mikoa hiyo, Magufuli aliwaahidi Watanzania kuwa atachapa kazi kwa uadilifu ili kuwaletea maendeleo kutoka pale alipoishia mtangulizi wake, Dk. Jakaya Kikwete.
Kwa nyakati tofauti tangu aanze kampeni mikoani, Magufuli amekuwa akiwaambia wananchi kuwa baada ya kumchagua yeye, wawachague wabunge wa CCM ili apate urahisi wa kuunda serikali na kuleta maendeleo.
Akiwa Sumbawanga Mjini katika Uwanja wa Nelson Mandela, Magufuli alifurahishwa na umati mkubwa uliojitokeza kisha akawaeleza vipaumbele vya serikali yake ya awamu ya tano.
Akiwa kwenye Jimbo la Kwela, Rukwa, aliwaahidi wananchi kuwa atafanya kazi vizuri kwenye utawala wake huku msafara wake ukisimamishwa na wananchi wa vijiji mbalimbali wakitaka kumsikia.
Akihitimisha ziara yake mkoani Rukwa, Magufuli aliahidi kuanzisha mamlaka maalumu ya kusimamia masilahi ya polisi.
Akiwa Mji wa Laela kabla ya kuelekea mkoani Mbeya, Magufuli alisema anataka kuboresha masilahi ya askari ili waache vitendo vya rushwa na kudhibiti wimbi la majambazi na wizi.
Akiwa katika Jimbo la Momba, Mbeya, Magufuli aliwata wananchi wa jimbo hilo wasifanye makosa safari hii, bali wakichague chama tawala.
Aliposimama katika Kijiji cha Ndalambo, Momba, Magufuli aliwaahidi wananchi wa eneo hilo kuwa ataunda serikali ya kuleta maendeleo ambayo hayatabagua watu kwa itikadi za vyama, dini, makabila wala mahali watokako.
Akiwa Tunduma mkoani Songwe, Magufuli alipata mapokezi makubwa hadi akasema: “Mapokezi haya ni ya hatari, ni tsunami. Kama ni ya namna hii leo nitalala kwa raha.”
Baadhi ya vipaumbele vya Magufuli ni pamoja na kuleta umoja wa kitaifa, kulinda Muungano, kuimarisha ulinzi na usalama, kuheshimu mihimili ya dola, kuunda mahakama maalum ya mafisadi na majizi, kusimamia utawala bora, kusimamia na kuheshimu mawazo yote ya kuleta maendeleo hata yakitoka upinzani na kuimarisha vyombo vya usalama.
Vingine ni kuongoza vita dhidi ya ubadhirifu, kusimamia ukusanyaji kodi na ilipwe na wote, kuongeza ajira kwa kuimarisha viwanda, sekta ya kilimo, mifugo, kudhibiti madini ili yalete maendeleo, kupeleka maji vijijini na mijini, kujenga zahanati kila kijiji, hospitali za rufaa kila mkoa, kuboresha masilahi ya wauguzi, elimu bure kuanzia shule ya msingi hadi kidato cha nne na vingine vingi.
Jana, Magufuli aliendelea na kampeni Mikoa ya Kanda ya Juu Kusini huku mgombea mwenza, Samia Suluhu akiwa Kanda ya Kaskazini.

Note: Only a member of this blog may post a comment.