Wednesday, December 2, 2015

Anonymous

SITTA, MWAKYEMBE Matatani? Wabunge na Posho, Makontena ya Dar? + Bilion 15 za TZ zilizopotea? – (Audio).

Kuperuzi na kudadisi @CloudsFM imekupita? Inawezekana hukuzipata zote zilizoweka headlines kwenye uchambuzi wa magazeti redioni asubuhi hii… kama ilikupita hizi ni dakika 20 za zile zote kubwa za leo.

Makontena 9 yakamatwa na TRA kwa ushirikiano na Jeshi la Polisi maeneo ya Mbezi Beach Tanki Bovu, Bosi TRA atajwa ufisadi wa mamilionikuanzia sasa ukitupa taka Dar es salaam faini Tzs. 50,000/- .

Serikali imeanza kuichunguza benki moja Tanzania na kampuni ya EGMA ya hapa nchini kutokana na kuhusika katika udanganyifu wa riba ya mkopo wa dola za Marekani Milion 600 sawa na Trilion 1.3 za kitanzania iliyopewa Tanzania na Benki ya Uingereza. 

Halmashauri ya Manispaa ya Ilala imesema itawachukulia hatua watu wote watakaotupa takataka ovyo kwa kuwatoza faini ya Tzs. 50,000/- kwa kosa hilo, Manispaa hiyo pia imeahidi kutoa zawadi ya Tzs 25,000/- sawa na 50% ya faini kwa mwananchi yoyote atakayesaidia kukamatwa kwa mtu atakayekutwa anatupa takataka ovyo.

Baadhi ya Wabunge, Wanasiasa na Wasomi nchini wamepongeza uamuzi wa Serikali kutowalipa posho Wabunge wanapofanya Ziara za kamati kwenye Taasisi na Mashirika ya umma kwenye maeneo yao… Waziri Mkuu mstaafu, Mizengo Pinda amekabidhi ofisi kwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Kassim na kumtaka aimarishe ufuatiliaji wa maelekezo anayotoa kwenda ngazi za chini.

Sauti yote  ya uchambuzi wa magazeti kwenye #PowerBreakfast ipo hapa chini, kusikiliza bonyeza play ikupeleke moja kwa moja.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.