SI YEYE TU
Kwa mujibu wa chanzo hicho, mbali na Wema, mastaa wengine ambao nao
magari yao yako kwenye orodha ya kuchunguzwa mwenendo wa kodi ni
Jacqueline Wolper Massawe (Toyota Prado), Kajala Masanja (Toyota Hilux)
na Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ (BMW X6).
“Unajua serikali imedhamiria kukusanya kodi. Anachotaka Rais Magufuli ni
kila mtu mwenye haki ya kulipa kodi ya kitu fulani, afanye hivyo bila
kukwepa. Na hakuna kumuonea mtu.
“Sasa bwana…bwana! Huko makao makuu (TRA) hakukaliki, huyo Kaimu
Kamishna Mkuu, Phillip Mpango ni mkali balaa, anadhani Magufuli
atamzukia wakati wowote wakati cheo kapewa juzi tu. Lakini nasikia
Magufuli anataka ripoti mezani kwake.
“Na ujue si magari ya hao mastaa tu ndiyo yako kwenye orodha, hata
watu wasio na majina hapa mjini, utaratibu umewekwa kuhakikisha magari
yote yanalipiwa kodi kama sheria inavyotaka. Kwa hiyo kama mtu ana
malimbikizo, imekula kwake, lazima alipe yote,” kilisema chanzo hicho.
WASIWASI WA VIPATO
Hata hivyo, chanzo hicho kilipoulizwa kama kuwabana mastaa kunatokana na
maisha yao ya kifahari huku vipato vyao vikiwa haviko wazi, alijibu:
“Ni zoezi. Linazingatia mambo mengi. Pengine hilo limo. Lakini ni zoezi
maalum.”
Ili kuthibitisha madai hayo, Amani lilianza kuwasaka mastaa hao, mmoja
baada ya mwingine ili kuona ukweli wa kuwepo kwa madai hayo.
WOLPER
Wolper alikuwa wa kwanza kutafutwa kwa simu ambapo alipopatikana alishtuka na kusema:
“Yesu! Sijafuatwa na mtu yeyote, lakini na mimi jana (Jumatatu)
nimeisikia hii. Lakini mimi nipo oke, ushuru nimeshalipa mwenyewe.
Kimbembe kipo kwa wale wenye mbwembwe ndiyo nasikia soo…Teh! Teh! Teh!”
KAJALA
Kajala alipotafutwa kwa njia ya simu ya mkononi juzi, hakupatikana hewani.
WEMA SASA
Amani likamsaka Wema ambaye kwa bahati njema alikuwa hewani na alipokea simu. Baada ya kusomewa madai hayo, alijibu:
Jamaa: “Ni jambo dogo tu, wala siyo ishu kubwa. Kwani nani kasema?”
Amani: “Tumezinyaka kivyetuvyetu.”
DIAMOND
Kwa upande wake, Diamond ilionekana kuwa ishu zaidi kwani, licha ya yeye
kutojibu meseji baada ya kutumiwa, BMW X6 lake linadaiwa bado lina deni
kutoka kwa mtu aliyemuuzia. Na mbaya zaidi, mtu huyo alifariki dunia
Aprili, mwaka huu
MANUNUZI YAO
Wema alisema Range lake alilinunua kwa dola za Kimarekani 90,000 (si
chini ya shilingi milioni 200). Diamond yeye awali alisema BMW hilo
alipewa na mameneja wake (Said Fella na Hamis Taletale ‘Babu Tale’)
ambao walilinunua kwa shilingi milioni 90.
Wolper yeye Prado lake aliliingiza ndani kwake kwa shilingi milioni 60 huku gharama ya gari la Kajala zikiwa hazijulikani.
Note: Only a member of this blog may post a comment.