King Kiki (kulia) akiimba sambamba na Aboubakar Kasongo Mpinda ‘Clayton’ enzi za uhai wake.
Aboubakar Kasongo Mpinda ‘Clayton’ akiwa na Issa Nundu (kulia).
Na Sifael Paul
Habari zilizoufikia mtandao huu zinaeleza kuwa
mwanamuziki mkongwe katika tasnia ya muziki wa dansi nchini mwenye asili
ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Aboubakar Kasongo Mpinda ‘Clayton’
amefariki dunia nyumbani kwake, Kinondoni jijini Dar.
Kwa mujibu wa wanamuziki waliofanya naye kazi kwa muda mrefu, Kasongo
ambaye alifanya kazi na bendi nyingi kama Maquis du Ziare akiwika na
Nyimbo za Angelo, Mwana Malole, Nasononeka, Baharia, Siri ya Mkoko na
zingine kibao amefariki dunia baada ya kuumwa kwa muda mrefu
akisumbuliwa na Kisukari hivyo taratibu za mazishi zinaendelea kufanywa
na familia yake.
Katika siku za mwishoni, Kasongo aliitumikia Bendi ya Bakulutu kabla
ya kujiunga katika Bendi ya Bana Maquis ikiwa chini ya Tshimanga Kalala
Asssosa.
Note: Only a member of this blog may post a comment.